Benki ya CRDB sasa kurahisisha wanafunzi kwenda mashuleni kwa wakati kupitia mkopo wa ‘ADA LOAN’. Mkopo huo wa hadi Shilingi milioni 12 ni mkombozi katika sekta ya elimu nchini kuanzia elimu ya awali mpaka elimu ya juu.
Mkopo huo unakwenda kusaidia wazazi, walezi na hata wanafunzi kukamilisha malipo yao ya ada kirahisi wakiwa popote kupitia app ya Simbanking. Huduma hii inapatikana kwa wateja wanaopitisha mishahara yao kwa benki ya CRDB tu.
Uzinduzi wa huduma hii uliongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mkuu wa Fedha, Benki ya CRDB Ndg. Fredrick Nshekanabo, Mkuu wa kItengo cha wateja binafsi Ndg. Stephen Adili, wafanyakazi wa benki pamoja na wageni waalikwa akiwemo Mkurugenzi wa Paradigm Schools Ndg. Mahmoud Mringo na wadau mbalimbali waliohudhuria wakiwemo wazazi, walimu na wanafunzi wa shule.