Mwigulu aipongeza TRA kuongeza makusanyo ya kodi.

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ameipongeza TRA kwa kuongeza makusanyo ya kodi kutoka sh. trillioni 22.2 mwaka wa fedha 2021/2022 hadi kufikia sh. trillioni 27.6 mwaka wa fedha 2023/2024 na kuvunja rekodi ya kukusanya sh. trillioni 16.528 katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2024/2025 kinachoanza Julai hadi Desemba mwaka 2024.

Alizungumza hayo wakati akifungua kikao kazi ch siku 5 kinachotathmini utendaji kazi wa nusu mwaka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano Arusha (AICC) jijini Arusha.

Aidha Dkt. Nchemba amesema kuwa fedha hizo zimesaidia Serikali kutekeleza miradi ya kimkakati inayolenga kuboresha huduma za jamii kama vile bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere, mradi wa treni inayoenda kasi (SGR), huduma za jamii na miundombinu ya barabara.

Dkt Nchemba amewaomba TRA kuimarisha zaidi mifumo ya kisasa ya kielektroniki ya kukusanya mapato ya Serikali ili kuongeza uwazi. Vilevile amewaomba TRA kutofunga biashara za watu wanaowadai kodi badala yake wawawekee utaratibu wa kuzilea biashara hizo huku wakihakikisha kodi stahiki zinalipwa na wahusika kwa kuwa vitendo vya kufunga biashara vinaathiri mfumo wa nchi pamoja na kuvuruga mfumo wa biashara husika na kuwasababishia watu umaskini na kuwakosesha wananchi ajira.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *