Fukuza Makocha bado inazidi kupamba moto na awamu hii Westham ya ligi kuu nchini Uingereza imemtimua kocha wake mhispanyola Julian Lopetegui ikiwa ni msimu wake wa kwanza akiwa kama kocha wa klabu hiyo.
Lopetegui aliyechukua mikoba ya kocha David Moyes amejikuta na mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha huku Westham wakionekana kupata wakati mgumu katika ligi hiyo nchini Uingereza.
Nafasi ya Julian Lopetegui itachukuliwa na aliyekuwa kocha wa Brighton na Chelsea, Graham Potter kuelekea mzunguko wa pili wa ligi hiyo.