Rais mteule wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kusomewa mashitaka katika kesi yake inayomhusu kulipa fedha kwa Star Stormy Daniels ili kumzuia kusema kuhusu uhusiano wa Kingono aliowahi kuwa nao dhidi ya Trump.
Jaji wa kesi hiyo Juan Merchan ameonyesha kuwa huwenda Trump asipewe kifungo cha jela, majaribio au faini lakini hatima yake itajulikana baada ya kikao hicho.
Kesi hii ni mfululizo wa kesi za jinai zinazomhusu Donald Trump ambaye anadai kuwa alilipa fedha kwa nia ya kulinda familia yake na wala sio kwaajili ya kampeni ya uchaguzi ingawa mashtaka hayo yanahusiana na kudanganya nyaraka za biashara.
Endapo hukumu hii itatolewa itamfanya Rais Donald Trump kuwa Rais wa kwanza wa Marekani kuhukumiwa kwa makosa ya uhalifu akiwa madarakani.